0
Watumishi 50 Wilaya Ya Makete Kusimamishwa Kazi Kwa Udanganyifu
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani  Njombe limepitisha na kuridhia kuwasimamisha kazi watumishi wapatao 50 waliojipatia ajira kwa njia ya udanganyifu na mtumishi mmoja aliyethibitika kuwa ni mtoro kazini .

Akitangaza mapendekezo ya kamati mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete mh Egnatio Mtawa  amesema hayo ni mawazo ya baraza la madiwani lilojigeuza kuwa kamati ili kuweza kujadili juu ya jambo hilo.

“Kamati imefikisha mapendekezo kwenye baraza kwamba wtumishi wapatao 60 watendaji wa vijiji,afisa mifugo mmoja,fundi sanifu mmoja na madreva wanne wathibitishwe kwenye ajira zao lakini pia kamati imependekeza watumishi wapatao 50 waliojipatia ajira kwa njia ya udanganyifu,na mtumishi mmoja ambaye amethibitika kuwa na utoro sugu kazini hao wote  kufukuzwa kazi”alisema Mtawa mbele ya kikao cha madiwani

Wakati huo huo  Mtawa amesema baraza limeunda tume ya uchunguzi wa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kupitia kwa watendaji wa vijiji na watendaji wa kata katika halmashauri ya wilaya hiyo.

“Lakini pia Baraza limewateu mh Jinson Mbalizi makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete,Abraham Okoka  mjumbe wa kamati ya fedha na mh.Atilio Ng’ondya diwani wa kata ya Mpungi hawa wawe ni wajumbe wa tume iliyoundwa kuchunguza  maswala ya utendaji kazi wa makusanyo kama ajenda ilivyofikishwa katika baraza letu”aliongeza mtawa wakati akisoma Mapendekezo.

Post a Comment

 
Top