Hayo yamesemwa na wananchi wa mtaa wa Mangula katika Halmashauri ya Mji wa Makambako mara baada ya kumkuta mtoto mchanga anayekadiliwa kuwa na miezi saba ambaye amewekwa kwenye ndoo na kutupwa na mama ambaye hajafahamika jina lake mpaka sasa katika eneo la uwanja wa amani mjini makambako.
Aidha mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mangula uliopo kata ya Mji mwema Roina Ngimbuchi amethibitisha kuokotwa kwa mtoto huyo, ambapo amesema kuwa mhusika wa tukio hilo mpaka sasa hajafahamika lakini serikali inaendelea na upelelezi wa kumbaini mtu ambaye amehusika na tukio hilo la kinyama linalo kiuka haki za watoto.
Mganga mfawidhi wa hospital ya Makambako Kesha mgunda amekiri kupokea mwili wa mtoto mchanga na kueleza kuwa mwili huo umehifadhiwa katika hospitali hiyo.
Hata hivyo mganga mfawidhi wa hospitali hiyo amewataka akina mama na wanawake wote kutumia uzazi wa mpango ili kuepukana na mimba zisizo tarajiwa ili kuepuka kufanya matukio yanayohatarisha uhai wa watoto.
Post a Comment