Trump ameandika leo katika ukurasa wake wa Twitter kwamba wawakilishi wake wameondoka Korea Kaskazini baada ya kufanya mazungumzo yaliyofanikiwa na wamekubaliana kuhusu muda na siku ya kufanyika kwa mkutano huo wa kilele kati yake na Kim.
Amesema mkutano huo wa pili kati ya viongozi hao utafanyika Februari 27 na 28. Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza mwaka uliopita huko Singapore.
Pia Trump amebainisha kuwa Korea Kaskazini chini ya uongozi wa Kim, itakuwa nchi yenye uchumi mkubwa zaidi. Kiongozi huyo wa Marekani amesema amejiandaa kukutana na Kim ili kuendeleza mchakato wa amani.
Post a Comment