TAKUKURU yamrejeshea Zitto simu yake ya mkononi
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema kuwa simu ya Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe iliyokuwa imeshikiliwa na TAKUKURU imerudishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ndg. Ado Shaibu amesema Zitto amepatiwa simu yake hiyo Alhamisi ya jana.
"Kitendo cha kushikilia simu yake kwa muda mrefu hakikuwa chenye afya lakini tunafurahi kuwa jana wamemrejeshea baada ya kuishikilia kwa siku nne," alisema Ado.
Disemba, 2019 Zitto alihojiwa na Takukuru pamoja na kutoa ushahidi wake kuhusu madai ya rushwa kwenye mradi wa Liganga na Mchuchuma akidai kuwa kuna kampuni tatu za chuma zinawahonga baadhi ya viongozi wa Serikali.
Baada ya kauli yake hiyo, Takukuru ilimuomba Mbunge huyo afike ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam ili kushirikiana kushughulikia suala hilo muhimu na takribani wiki moja iliyopita simu yake ikachukuliwa.
Post a Comment