Mwanasheria huyo Mkuu wa CHADEMA kwenye mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya America (VOA) amesema kuwa hiyo itakuwa ni operesheni ya 23 tangu aliposhambuliwa kwa risasi.
"Naweza kusema naendelea vizuri, sijapona kwa sababu tarehe 20 ya mwezi huu ninaenda kufanyiwa operesheni nyingine ya 23, kwa hiyo sijapona lakini naendelea vizuri," amesema Lissu.
Utakumbuka Septemba 17, 2017 Tundu Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi
akitokea Bungeni Jijini Dodoma. Lissu alipatiwa matibabu ya mwanzo Nairobi nchini Kenya kisha
kuhamishiwa Ubelgiji.
Post a Comment