Serikali imetoa rai kwa waendesha bodaboda kote nchini kujiunga katika vikundi hali itakayowawezesha kutambulika vizuri na kupatiwa mikopo.
Rai hiyo imetolewa leo Februari 6 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira na vijana ,Antony Mavunde wakati akijibu swali la mbunge wa Lushoto Shaban Shekilindi aliyehoji kwa kuwa bodaboda imetoa ajira kwa vijana wengi,kuna mpango gani wa serikali kuwawezesha mikopo vijana wa bodaboda.
Naibu waziri Mavunde amesema serikali inashirikiana na serikali za mitaa ili vijana kujiunga katika vikundi na kutengeneza katiba ya vikundi husika ili waweze kupatiwa mikopo na amesisitiza kuwa serikali hutoa mikopo kama vikundi vya bodaboda vitaonesha utayari huo
Mbunge wa viti maalum [CHADEMA]Suzan Lyimo naye amehoji licha ya bodaboda kutambuliwa kama kazi maalum kwanini serikali imekuwa ikiwakataza kufanya shughuli katika miji yenye misongamano mikubwa ya watu hususan katikati ya jiji la Dar es Salaam na eneo la chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Katika majibu yake Mhe.Mavunde amesema kuwa suala la kuwazuia bodaboda lilikuwa ni suala la kiusalama na msongamano lakini serikali inafanya namna ya kuwasaidia hususan kwa kutambua vituo rasmi vya maegesho.
Katika Bunge la 11 ,mkutano wa 14 kikao cha 8 ,Jumla ya Maswali 16 yameulizwa pamoja na hati mbili za taarifa kuwasilishwa bungeni ambazo ni taarifa ya kamati ya Nishati na Madini ya mwaka 2018/2019 na taarifa ya kamati ya mambo ya nje ,ulinzi na Usalama ya mwaka 2018/2019.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment