Mgumba alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kuteuliwa (CCM) Abdallah Bulembo bungeni leo, Alhamisi Februari 6 mwaka 2019.
“Wakulima wana shida, kahawa yao iko katika maghala hawajalipwa hadi leo. Kwa nini Serikali isifanye kama ilivyofanya katika korosho?” Amehoji Bulembo.
Akijibu swali hilo, Mgumba amesema Serikali haijanunua kahawa ya wakulima na kwamba wakulima waliamua wenyewe kupitia vyama vyao vya ushirika kuuza kahawa yao mnadani Moshi.
Amesema kutokana na kuyumba kwa soko la dunia na kuongezeka kwa uzalishaji bei ya zao hilo imepungua.
Post a Comment