0
Rais Museveni akataa wanawake kutumika kama kivutio cha utalii
Rais wa Uganda,  Yoweri Museveni  amepinga pendekezo Wizara ya Utalii la kutumia wanawake wenye maumbo mazuri (curvy women) kama kivutio cha watalii nchini humo.
Asema pendekezo hilo halijapitishwa na baraza la mawaziri, na hawezi kuruhusu wanawake kuonesha miili yao kwa watalii.

Utakumbika hivi karibuni Wizara ya Utalii nchinoi humo ilizindua shindano la kuwapata wanawake hao watakaowavutia watalii, shindano hilo linajulikana kama  Miss Curvy Uganda.

Waziri wa utalii nchini humo, Godfrey Kiwanda alipendekeza kuwe na onyesho la wanawake wenye maumbo makubwa ili kuvutia wageni zaidi wanaoitembelea nchi hiyo. Hata hivyo Kauli hiyo haikupokelewa vyema nchini humo hasa kwenye mitandao ya kijamii

Post a Comment

 
Top