Kumekuwa na mjadala nchini Tanzania na zaidi katika mitandao ya kijamii baada ya mbunge mmoja kulishauri bunge kuweka utaratibu maalum kukagua wanaume walio na 'mkono sweta' au wanaume ambao hawajatahiriwa.
Mbunge maalum Jackline Ngonyani amependekeza hatua hiyo katika hoja ya kujadili udhibiti wa maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini.
Akizungumza bungeni, Mbunge huyo ameeleza bunge kwamba lengo la 90-90-90 la virusi vya ukimwi litafikiwa nchini Tanzania, pale kutakuwa na ridhaa ya watu kujipima wenyewe.
'Nawashtaki wazazi wangu kwa kunizaa'
Ameeleza kwamba changamoto kubwa ni kutokana na kuwa baadhi ya watu wanoana aibu kupimwa vituoni, hasaa wanaume.
Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na VVU/AIDS (UNAIDS) na washirika wake, walizindua lengo la 90-90-90 ambalo limenuia; kutambua kwa 90% watu wote walioathirika na virusi vya Ukimwi, kutoa matibabu ya dawa za kuzuia makali ya VVU kwa 90% ya waliotambuliwa, na kufanikiwa kudidimiza kusambaa kwa virusi kwa 90% kwa waliotibiwa kufikia 2020.
Bi Ngonyani amependekeza, 'Nashauri tuanze na wabunge humu ndani ambao watabainika hawajafanya hiyo tohara ili wafanyiwe tohara mara moja'.
Mbunge huyo amesisitiza kwamba wengi wanaona aibu kwenda kupima, lakini iwapo kutakuwa na utaratibu unaofuatwa wa kila mmoja kujipima mwenyewe itakuwa ni vyema na kusaidia kupunguza kusambaa kwa virusi vya ukimwi nchini.
Wabunge Tanzania wapimwa virusi vya HIV
Utafiti uliofanywa kwa wingi kweli, umebaini kwamba wanaume ambao hawajatahiriwa wana nafasi ya kuambukizwa na kuenezea maambukizi mbali mbali ikiwemo ya ugonjwa wa ukimwi.
Shirika la afya duniani WHO linasema kupasha tohara kunapunguza hatari ya wanaume kuambukizwa virusi vya Ukimwi kwa a
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment