0
Klabu ya African Lyon waiandikia barua bodi ya ligi kuu Tanzania bara
Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) imeandikiwa barua na Klabu ya African Lyon kuomba mchezo wao namba 271 dhidi ya Simba SC uhamishiwe Dar es Salaam.

Klabu hiyo wamefikia maamuzi hayo ambapo awali walikuwa wanatumia Uwanja Sheikh Amri Abeid Arusha kwa mechi za nyumbani.

Mwanzoni Lyon waliandika Barua kuomba mechi zao za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe Sheikh Amri Abeid Arusha na Bodi ya ligi ilibariki maabadiliko hayo.

Taarifa imesema kuwa Lyon inadai mchezo dhidi ya Yanga ambao ulifanyika mkoani Arusha katika dimba la Sheikh Abeid Arusha December 20 na Lyon kufungwa kwa goli moja kwa bila (1-0) walipata hasara kutokana na gharama za kambi.

Ukiachana na kambi, gharama za usafiri na pia makato mbalimbali ilikuwa hasara kwao ndiyo maana wameomba mchezo wao dhidi ya Simba ambao utachezwa February 19 ufanyike katika dimba la Taifa, Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top