0
Kesi ya Kitilya na Wenzake yatinga Mahakama ya Uhujumu Uchumi
Upande wa Jamhuri umeshawasilisha jalada la kesi ya  Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya na wenzake.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 58 yakiwamo 49 ya kutakatisha fedha.

Jalada hilo limewasilishwa katika mahakama hiyo jana likiwa na taarifa ya maelezo ya mashahidi na kupokelewa kisha kurejeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa hatua za mwisho ili ianze kusikilizwa.

Washtakiwa wanasubiri kuitwa na Mahakama ya Kisutu kwa tarehe itakayopangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya mashahidi kisha jalada lirudi Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni, Kitilya, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda, msaidizi wake Alfred Misana na maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.

Post a Comment

 
Top