0



Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imesema kanuni ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) inayoweka utaratibu wa kusimamia vibali vya kumbi za sanaa na burudani inakwenda kinyume na sheria ya baraza hilo.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo leo Ijumaa Februari 8, 2019 mwenyekiti wa kamati hiyo, Andrew Chenge amesema pia hatua hiyo inafanya watoa huduma za kumbi hizo kuingia gharama mara mbili kwa kuwa halmashauri nazo zimekuwa zikitoza ushuru mbalimbali kupitia huduma hizo.

“Hii inaweza kupelekea kuongezeka kwa gharama za kukodi kumbi za maonyesho ya sanaa na burudani,” amesema.

Post a Comment

 
Top