0
Ikulu yanena kutumbuliwa Balozi
Baada ya kusambaa mitandaoni kwa taarifa ya kutumbuliwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilsoni Masilingi ikulu imetoa ufafanuzi wa kwamba barua hiyo siyo ya kweli.


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii (Twitter) na kusema kwamba barua hiyo haina ukweli wowote.

"Imeghushiwa, tafadhali ipuuzeni. 'Fake, please ignore'".

Barua ya kutenguliwa kwa uteuzi wa Balozi Masilingi imeanza kusambaa ikiwa ni siku moja tangu kukutana na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu katika kituo cha utangazaji VOA nchini Marekani.



Post a Comment

 
Top