0
Husna Afunguka Kuibiwa Bwana na Tunda
KUTOKANA na habari kuzagaa mitandaoni kuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid ameibiwa bwana na video queen wa Bongo, Tunda Sebastian anayejulikana kwa jina la Ally, hatimaye mwanadada huyo ameibuka na kufunguka.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Husna alisema watu wamekuwa wakizungumza sana kuhusiana na hilo kwamba ameibiwa bwana na rafiki yake Tunda kitu ambacho hakifahamu kwani anachojua yeye ni kwamba ana mpenzi wake mmoja tu anayejulikana kwa jina la G na ndiye rafiki yake pia. “Jamani naomba watu waelewe kwamba nina mpenzi wangu anaitwa G, huyo mwingine anayetajwa simjui na wala sina urafiki na mtu zaidi ya mpenzi wangu, huyo ndiye rafiki yangu wa karibu,” alisema Husna

Post a Comment

 
Top