0
Bwana mmoja nchini India apanga kuwashtaki wazazi wake kwa Kumzaa

Bwana mmoja mwenye miaka 27 nchini India anapanga kuwashtaki wazazi wake kwa kumzaa bila ridhaa yake.

Bwana huyo aitwae Raphael Samuel ambae ni mfanyabiashara ameiambia BBC ya kuwa si sahihi kuzaa watoto kwa sababu watapambana na magumu ya maisha katika umri wao wote watakaoishi duniani.

Bw Samuel, yumkini anafahamu kuwa ridhaa haiwezi ombwa kabla ya kuzaliwa, lakini anasisitiza kuwa, "hayakuwa maamuzi yetu kuzaliwa".

"Hivyo, hatukuomba kuzaliwa. Inabidi tulipwe kwa maisha yetu yote ili tuishi,"

Madai kama haya yanaweza kuzua mgogoro kwenye familia yeyote ile, lakini Bw Samuel ana mahusiano mazuri na wazazi wake, ambao wote wawili ni wanasheria, na wanalichukua suala hilo kama kichekesho.

Bi Kavita Karnad ambaye ni mama mzazi wa bwana huyo imebidi atoe tamko kutokana na "kadhia aliyoianzisha mwanangu hivi karibuni."

"Kwanza, navutiwa kwa ujasiri aliouonesha mwanangu kwa kutaka kutupeleka mahakamani akijua fika kuwa sisi ni wanasheria. Na iwapo Raphael atatupa maelezo yenye mashiko juu ya namna gani tungepata idhini yake kabla hajazaliwa, basi nitakubali makosa yangu," amesema mama huyo kwenye taarifa yake.


Imani hiyo ya Bw Samuel inatokana na filosofia anaoifuata ijulikanayo kama anti-natalism - ambayo inafundisha kuwa maisha yamejaa shida tupu na hivyo watu waache kuzaana mara moja.

Hilo likiwezekana, basi taratibu binadamu wataondoka kwenye uso wa dunia halia mabayo itaikoa sayari hii.

"Hakuna haja ya kuwa na binaadamu. Watu wengi wanateseka na shida za dunia. Iwapo wataisha, dunia na wanyama watakuwa ni wenye furaha kabisa, maana watastawi. Pia hakutakuwa na binaadamu watakaoumia kwa shida na madhila. Maisha ya binaadamu hayana maana kabisa."

Mwaka mmoja uliopita, alianzisha ukurasa wa Facebook uitwao Nihilanand, amabao una picha kadhaa akiwa na ndevu ndefu za bandia na mabango tele ya ujumbe wa filosofia yake.

"Kulazimisha mtoto azaliwe na kumlazimisha awe na kazi ni sawa na kumteka na utumwa tu?" ni moja ya mabango yake na pia, "Wazazi wako walikuzaa wewe badala ya kunua mwanasesere ama kufuga mbwa. Hawakudai chochote, wewe ni starehe yao tu ."

Post a Comment

 
Top