Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amepata shavu la maana Baada ya kushirikishwa kwenye Albamu mpya ya Msanii wa muziki kutoka Nigeria Timaya.
Album mpya ya staa Timaya wa Nigeria inayoitwa ‘Chulo Vibes’ ikiwa na jumla ya ngoma tisa ambapo imewashirikisha wasanii tofautitofauti akiwemo BurnaBoy,Machel Montano.
Kupitia ukurasa wa instagram wa Timaya ameweka cover ya Album yake bila kutaja tarehe rasmi ya kuichia sokoni huku ngoma yake na Alikiba ‘Number One’ ikishika nafasi ya tano ndani ya Album hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment