0
Zahera aipelekea maumivu Simba
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema hawezi kuumizwa na timu yake kutolewa kwenye michuano ya SportsPesa kwasababu bado kuna timu za Tanzania kwenye michuano hiyo.



Zahera amesema licha ya timu yake na Singida United kutolewa lakini anaamini Tanzania bado inaweza kulibakiza kombe hilo nyumbani kutokana na uwepo wa timu za Simba na  Mbao FC ambazo zinacheza leo.

''Mimi siwezi kuumia kwasababu tumetolewa ila nawatakia Simba watuwakilishe vizuri ili waifunge AFC Leopards na waende fainali wakachukue ubingwa huo ili usiondoke Tanzania'', amesema Zahera.

Leo kutakuwa na michezo miwili ya SportPesa Cup ambapo Tanzania itawakilishwa na timu mbili, Mbao FC ikicheza na Gor Mahia saa 8:00 mchana wakati Simba yenyewe itacheza na AFC Leopards saa 10:00 jioni.

Yanga jana ilitupwa nje ya michuano hiyo kwa kufungwa mabao 3-2 na Kariobangi Sharks kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo.




Post a Comment

 
Top