Tume ya kutetea kutetea haki za binadamu nchini Zimbabwe limewatuhumu maafisa wa usalama kwa kutumia "utaratibu wa mateso" kuzima maaandamano.
Ghasia zilizuka zaidi ya wiki moja iliyopita kufuatia hatua ya serikali ya kuongeza bei ya mafuta.
Msemaji wa serikali ametetea msako huo, ameiambia BBC: "Mambo yakiharibika wakati mwingine unahitaji kutumia nguvu kiasi."
Ripoti zimeibuka kuwa wanajeshi wanadai kuwapiga na kuwaumiza watu katika maeneo tofauti ya mji mkuu wa Harare.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding alizungumza mmoja kati ya wanaume 30 waliyokamatwa na kupigwa na maafisa wa polisii.
''Kuongezeka kwa hali ya ghasia nchini Zimbabwe kumeibua maswali kuhusu uwezo wa rais Emmerson Mnangagwa kudhibiti majeshi yaliyomweka madarakani miezi 14 iliyopita.'' aliongeza mwandishi wetu.
Rais Mnangagwa ameahidi kuwa visa vya dhulma dhidi ya wanainchi havitakubaliwa.
Katika taarifa yake, tume hiyo imesema kuwa karibu watu wanane wameripotiwa kufariki kutoka wiki iliyopita, "hususana kutokana na majeraha ya risasi".
"Maafisaa wa vikosi vya jeshi la Zimbabwe na polisi waliyojihami wamekuwa wakiwatesa watu.
Mateso hayo yaliyopangwa yanalenga wanaume wanaoishi karibu na maeneo yaliyowekwa vizuizi vya barabarani vilivyochomwa na waandamanaji au wezi," ilisema taarifa hiyo.
Mitandao ya kijamii kudhibiti maudhui zaidi
Tume hiyo iliangazi kwa kina katika ripoti yake jinsi maafisaaa wa usalama walivyokua wakiingia nyumba za watu usiku na kuwapiga wanaume na wavulana wadogo wa hadi miaka 11.
"Hatua ya kupeleka wanajeshi kutuliza maandamano husababisha maafa makubwa na ukiukaji wa haki za binadamu''iliongeza ripoti hiyo
Rais Mnangagwa amesema nini?
Siku ya Jumatatatu Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alilazimika kukatiza ziara yake barani Ulaya na kurejea nyumbani kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.
Alitarajiwa kuhudhuria kongamano la kimataifa la kiuchumi mjini Davos Uswizi ili kutafuta waekezaji nchini Zimbabwe.
Alipofika mjini Harare, kupitia mtandao wake wa Twitter, alitoa wito kwa pande zinazozona kuungana katika juhudi za kuimarisha uchumi wa taifa uliyozorota.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment