0
Ufaulu Waongezeka Huku Shule Moja Yafutiwa Matokeo
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38, huku likifuta matokeo ya shule moja.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dkt. Charles Msonde , amesema kuwa wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari  ya Malinyi mkoani Morogoro wamefutiwa matokeo hayo baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.

"Mbali na kufuta matokeo hayo, NECTA imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani, kutokana na udanganyifu huo", amesema Dkt. Msonde

Dkt. Msonde amesema kuwa wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.

Post a Comment

 
Top