0
Rais Magufuli: Hakuna Mwanasiasa Aliyezuiliwa Kufanya Mikutano Kwenye Eneo Lake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema hakuna kiongozi wa kisiasa ambaye amezuiliwa kufanya mikutano kwenye eneo lake ambalo amechaguliwa na kusema hali hiyo ndiyo demokrasia.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na viongozi wa madhebebu mbalimbali ya dini ili kujadili masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

Akijibu swali la mchungaji Lyimo ambaye aliohudhuria hafla hiyo, Rais wa Magufuli amesema hakuna mtu aliyezuiliwa kufanya mikutano kwenye maeneo yao bali lengo ni kuhakikisha waliochaguliwa na wanapewa nafasi.

Alibainisha, hakuna mikutano iliyozuiliwa bali baada ya uchaguzi kila aliyeshinda anatakiwa afanye mikutano katika eneo lake bila kuingilia wengine kwa lengo la kudumisha amani na kuwapa watu muda wa kufanya kazi.

“Demokrasia si kuruhusu maandamano tu na demokrasia ina mipaka yake, hatuwezi kuruhusu watu wawe wanaandamana
tu na kutukana. Tukienda kwa utaratibu huo tutashindwa kuitawala nchi na tutashindwa kufanya mambo mengine,” alisema Rais Magufuli na kusisistiza:

“Hakuna aliyezuiliwa kwenda kufanya mikutano mahali pake na wapo wanafanya hata ninyi (viongozi wa dini) mmeshuhudia.

"Tunataka kama viongozi wa dini mnavyoheshimiana na usivyoweza kwenda kwenye kanisa la mwenzako na kuanza kutoa maneno, ndivyo hivyo na vyama vyetu viheshimiane. Hiyo ndiyo ninayoamini ni demokrasia nzuri ya kufanya kazi kwenye eneo lako.”

Aidha, viongozi hao wa dini pamoja na mambo mengine walimpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya hasa ya kujali maslahi ya wanyonge .

Rais Magufuli, alisikiliza michango kutoka kwa viongozi 42 ambapo pamoja na kumsifu kwa mambo mazuri aliyofanya kila mmoja alieleza changamoto za taifa na zile zilizowahusu wao binafsi.

Post a Comment

 
Top