0
Rais Magufuli Akutana na Viongozi wa Dini Ikulu Dar
Nimeona tujaribu kuukaribisha mwaka kwa namna nyingine kwa kuwakaribisha viongozi wa dini tuzungumze mambo mbalimbali na kuwasikiliza ninyi kwani ndio mnaotuongoza kiroho, niliona hii inaweza kuwa nafasi ya kupata ushauri kutoka kwenu.” – Rais Dk. Magufuli.



“Ninataka mjisikie mko huru wote na ndio maana imekua ngumu kuchagua nani atuongozee maombi lakini ninajua mbele ya Mungu wote mko sawa. Kwahiyo ndugu zangu ninawashukuru sana najua mneniombea sana,kila mara nilipokuwa nikisema naomba mniombee nimekuwa nikifatilia kweli mmeniombea sana,nawashukuru sana.” – Rais Dk. Magufuli.



“Nimekuwa nikifuatilia mahubiri mbalimbali kwenye vyombo vya habari, mpaka yule mchungaji anaitwa nafikiri Denis Mgogo ambaye anasema mwenge mtumie kama ‘opportunity’ kwamba muache kulalamika kama nivyuma vitawabana mpaka mtaitika Abee”. – Rais Dk. Magufuli.



“Mimi sijawahi kukaa Ikulu kabla, kwa hiyo sijui lakini inaweza ikawa ndio mara ya kwanza kwa Viongozi wote wa kidini, wengi namna hii kutoka kwa kila dhehebu, huu unaweza kuwa mwanzo mzuri.” – Rais Dk. Magufuli.



“Rais tuliyekuwa tunamuomba ni wewe, nimeanza kukuombea tangu ukiwa Waziri wa Ujenzi na leo umekuwa Rais bado nakuombea na tunawaza 2025 baada yako itakuwaje, maana tunahitaji Kiongozi kama wewe.” – Mchungaji Amani Lyimo.



“Mheshimiwa Rais Magufuli, suala la Demokrasia ni muhimu, watu wana hofu hata kama huambiwi na watendaji wako, kama kazi baba unapiga kweli wewe waachie wazungumze maana Watanzania hawatachagua maneno bali watachagua kazi, wape uhuru waseme.  – Mchungaji Amani Lyimo.



“Mchungaji Lyimo ameshauri ziwekwe sheria ili madhehebu yapungue, mimi nina mawazo tofauti na yeye, ukiangalia baa zipo nyingi hadi wengine wananywea chini ya mti, na pombe imesemwa kwenye vitabu vya dini siyo nzuri kwetu sote, Wakristo na Waislam.”  – Askofu Josephat Gwajima.



“Pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar kuna msikiti kwa ajili ya Waislam, nilikuwa naomba pia kujengwe pia Kanisa kwa ajili ya Wakristo kuabudu ili kuleta usawa. Suala la kuabudu ni muhimu sana katika mazingira ya kazi.”  – Askofu Josephat Gwajima.



“Umefanya jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia, tumekuja kwa pamoja na kwa upendo kujadili mambo ya mbalimbali ya nchi Mungu atakusaidia sana na kukuinua sana katika utawala wako” – Askofu Josephat Gwajima.



“Mh. Rais Magufuli Mungu kakutengeneza kuwa madini bora katika madini, ukiona mtu anawajali sana wanyonge, basi fahamu kwamba huyo ni madini bora, wewe ni madini bora”. – Sheikh – Hassan Said Chizenga.



“Kwenye Biblia na Quran imeandikwa kamari ni haramu, lakini hapa TZ saivi Vijana wanacheza kamari kupitia Mitandao ukifungua TV unakuta matangazo, haya Makampuni wao ni hapa kamari tu, matatizo nguvu kazi yetu inacheza kamari.” –Kiongozi wa Dini ya Mabohora.



“Changamoto inatokea pale Kanisa linapotaka kujenga hosipitali, Serikali nayo inataka eneohilo hilo, tunafahamu ushirikiano wa Serikali na Taasisi binafsi (PPP) katika masuala ya maendeleo.” –

Post a Comment

 
Top