0
Polisi Yafunguka Kuhusu Makamanda Watatu na Waziri Lugola Waliotumbuliwa na Waziri Lugola
Jeshi la Polisi nchini limesema taarifa za utenguzi wa makamanda watatu iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola wameipokea na wanaifanyia kazi.



Akizungumza na Waandishi wa Habari katika makao Makuu ya Jeshi hilo Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, DCP Ahmed Msangi amesema taarifa za Utenguzi wa makamanda hao zimekwishafika mezani kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro na zinafanyiwa kazi.



Aidha Kamanda Msangi ametoa taarifa kuhusu hali ya usalama nchini ambapo amesema ni shwari na vyombo vya ulinzi vinashirikiana na wananchi kutokomeza uhalifu huo.



Katika hatua nyingine Kamanda Msangi ametoa tathmini ya chaguzi ndogo zilizofanyika mwisho mwa mwaka jana na kusema chaguzi hizo zimemalizika salama na kutoa pongezi kwa Tume ya Uchaguzi kwa kusimamia chaguzi hizo kwa ufanisi.



“Ikumbukwe kuwa jukumu kuu la Jeshi la Polisi ni kulinda maisha ya watu na mali zao kuhakikisha kuwa wahalifu wa aina zote wanadhibitiwa ipasavyo,” amesema Msangi.

Post a Comment

 
Top