MSANII wa Marekani, Christopher Maurice Brown maarufu kama Chris Brown, anaandamwa na tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 huko Ufaransa usiku wa Januari 15 mwaka huu.
Mwanamke huyo amesema kwamba alifanyiwa tukio hilo baada ya kukutana na msanii huyo club huko ufaransa, na akamkaribisha chumbani kwenye hoteli aliyofikia iliyokuwa inajulikana kwa jina la ‘Mandarin Oriental Hotel.Mwanamke huyo amefunguka kwamba chumba walichotumia na Chris Brown ndipo alipomfanyia kitendo hicho humo.
Chris Brown (Breezy) hajasema neno lolote juu ya taarifa hizo.
Taarifa zilizotolewa na chanzo cha Ufaransa cha ‘Closer’, kinaeleza kwamba Breezy yupo chini ya upelelezi wa polisi kuhusiana na tuhuma hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment