Mchungaji Lyimo amesema hayo leo Jumatano Januari 23, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam katika kikao kati ya Rais Magufuli na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini.
“Rais tuliyekuwa tunamuomba ni wewe, nimeanza kukuombea tangu ukiwa Waziri wa Ujenzi na leo umekuwa Rais bado nakuombea na tunawaza 2025 baada yako itakuwaje, maana tunahitaji Kiongozi kama wewe.
“Mheshimiwa Rais Magufuli, suala la Demokrasia ni muhimu, watu wana hofu hata kama huambiwi na watendaji wako, kama kazi baba unapiga kweli wewe waachie wazungumze maana Watanzania hawatachagua maneno bali watachagua kazi, wape uhuru waseme." – Amesema Mchungaji Amani Lyimo.
Post a Comment