0
Mariah Carey Amshtaki Msaidizi Wake Kisa Hiki Hapa
MWIMBAJI Mariah Carey wa Marekani amemshtaki msaidizi wake wa zamani, Lianna Azarian, kwa kumrekodi kwa video mambo matukio ya “maudhi” na kisha kumtishia kwamba atazisambaza video  hizo kama hatamlipa Dola milioni nane.

Kwa mujibu wa hati za mahakamani Carey alisema alimwajiri Azarian mnamo Machi  2015 ambapo alianza njama za kununua vitu kwa kutumia kadi maalum ya  bosi wake  akidai alikuwa anafanya hivyo kwa kutumwa.  Pia alifanya mambo mengine ya kutumia jina lake kwa ajili ya kujinufaisha.

Pia hati hiyo inasema Azarian alikuwa akimpiga picha za siri za “mambo binafsi”  Mariah ambazo zinaweza kuwa za “maudhi” na kumvunjia heshima iwapo zitasambazwa.




Mariah alimfukuza kazi Azarian mnamo Novemba 2017 ambapo alikuwa anamlipa Dola 327,000 (Sh. mil. 752.8)kwa mwaka kabla ya hapo.  Alisema Azarian alianza vitisho hivyo baada ya kufukuzwa kazi.

Hati ya mashtaka haisemi kilichopo katika video hizo, lakini inasema kuna mambo mengine “binafsi”.

Mariah anadai kulipwa zaidi ya Dola milioni tatu (Sh. bil. 6.7).

Post a Comment

 
Top