0
Majeraha Yamsababisha John Boko Kushindwa Kwenda Congo
Nahodha na Mshambuliaji wa Simba SC, John Bocco ameachwa na kwenye kikosi cha timu hiyo
kilichosafiri kuelelekea DR Congo kuivaa AS Vita.

Simba SC itacheza mechi yake ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi wiki hii mjini Kinshasa dhidi ya wenyeji, AS Vita ambao mechi yao ya kwanza walifungwa 2-0 na wenyeji, Al Ahly nchini Misri.

Daktari wa Simba SC amesema Bocco atakuwa nje kwa siku 10 baada ya kuumia kwenye Jumamosi
iliyopita kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D dhidi ya JS Saoura.

Post a Comment

 
Top