0
Amuua Mke wake kisa kulazimisha kumpeleka mtoto Shule
Mkazi wa Kijiji cha Busale Kata ya Busale wilayani Kyela mkoani Mbeya, Zawadi Daudi ( 41), anadaiwa kuua mkewe, Hawa Kamwela (32), kwa kumcharanga kwa panga kwa madai kuwa anamlazimisha kumpeleka mtoto shule kuanza kidato cha kwanza.

Jirani wa mtuhumiwa, Said Mumba, alisema mgogoro kati ya mtuhumiwa na mkewe ulianza baada ya mtoto wao, Siri Zawadi (14), alipochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mkewe na mkewe kumweleza wafanye maandalizi.

Alisema wakati mama wa mtoto huyo akimweleza mumewe waanze maandalizi ya mtoto kwa kumnunulia mahitaji ya shule, mumewe alisema hana pesa na hayuko tayari kumpeleka mtoto shule, na kuwa baada ya hapo mwanamke huyo alikwenda kushtaki katika ofisi ya kata akitaka kujua sababu ya mumewe kukataa.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Aida Maonwa, alisema alipata mshtuko baada ya mtuhumiwa kufanya mauaji hayo na kwamba chanzo chake ni mtuhumiwa kugoma kumpeleka mtoto shule kwa madai hana pesa za kumnunulia mahitaji.

Alisema baada ya kesi kufika ofisi ya kata, mtuhumiwa aliitwa, lakini hakufanya hivyo na alipotafutwa alikuwa akipiga chenga, akitaka shauri hilo lipelekwa mahakamani ambapo mahakama ilimtumia wito, lakini hakufika na alipofuatwa nyumbani hakuonekana.

Post a Comment

 
Top