0
Aliyekuwa Kamishna Mkuu TRA Kitilya na wenzake kusomewa maelezo ya mashahidi Feb.8
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 8, mwaka huu kuwasomea maelezo ya mashahidi (commital) aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na mwenzake wawili wanaokabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya jana upande wa utetezi kueleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kupinga maombi ya upande wa mashtaka ya kutaka kesi hiyo ihairishwe kwa siku 14 wakieleza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kufaili taarifa hivyo wanaomba siku hizo kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Masumbuko Lamwai ulidai, kuwa washtakiwa hao wamekaa ndani kwa miaka mitatu, kisha kesi hiyo ikafutwa kiujanja ujanja na kuileta tena hivyo wanashangaa ni kitu gani kinakwamisha watu hao wasisomewe maelezo ya mashahidi.

“Watu hawa wameshakaa ndani miaka mitatu sasa, walifutiwa kesi kiujanja na kuleta tena kesi hii ili wakae tena ndani, hivi ni kitu gani kinazuia commital (maelezo ya mashahidi), alidai na kuongeza kuwa ...Wiki iliyopita walisema leo (Jana) watawasomea na sasa wanasema wapo kwenye hatua za mwisho watueleze hiyo hatua,”.

Awali Wakili wa TAKUKURU Leonard Swai alidai, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa wanaomba tarehe nyingine ili wakamilishe zoezi la kuwasilisha taarifa kwani wapo katika hatua za mwisho.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na Msaidizi wake Alfred Misana.

Katika mashtaka hayo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu, 49 utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na shtaka moja la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.

Wanadaiwa kati ya Machi 15, mwaka 2013 na Januari 10, mwaka 2014 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya washtakiwa wote walijipatia Dola za Kimarekani Milioni sita wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.
Advertisement
advert
==



Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

Give your exterior walls a unique look
Monitor
|
Sponsored
Virtually Indestructible Drone Takes Tanzania, United Republic Of By Storm
DroneX Pro
|
Sponsored
Cloud storage; five of the very best compared
PCW
|
Sponsored
7 Foods to Avoid a Deadly Blood Clot
Health & Human Research
|
Sponsored
Finally. The Smart Watch Every Man In Tanzania, United Republic Of Has Been Waiting For!
Tact Watch
|
Sponsored
11 Cancer Symptoms You Are Probably Ignoring
Stay Fit, Stay Active
|
Sponsored
10 Easy Skin Secrets Dermatologists Don’t Want You to Know
Womensarticle.com
|
Sponsored
7 Drinks to Help Ease Arthritis Pain
Health & Human Research
|
Sponsored
.....


===

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )


Batuli 'Amwaga Machozi' Baada ya Picha zake za Nusu Uchi Kusambazwa MitandaoniMPEKUZI: Batuli 'Amwaga Machozi' Baada ya Picha zake za Nusu Uchi Kusambazwa Mitandaoni
Entertainment News,Politics News ,Celebrity Gossip and Live Updates,United States, United Kingdom Batuli  'Amwaga  Machozi'  Baada  ya  Picha  zake  za  Nusu  Uchi  Kusambazwa  Mitandaoni
MPEKUZI


Home
View web version
Jackline Wolper: Msaka Pesa toka Machame aliyeishia kwa Matapeli wa Mapenzi jijini DarMPEKUZI: Jackline Wolper: Msaka Pesa toka Machame aliyeishia kwa Matapeli wa Mapenzi jijini Dar
What Happens to

Post a Comment

 
Top