Watu wanne wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa kutokana na ajali ya basi la Fikoshi linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Mwanza, iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Uvinza mkoani Kigoma.
Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa basi hilo, na kusababisha kupinduka lilipokuwa likipita kwenye eneo la Uvinza ambalo lina kona nyingi kali.
“Ajali imetoka jana usiku maeneo ya Uvinza kuna sehemu inaitwa Mnarani, ni barabara ya Vumbi, ilipofika maeno hayo ambayo ina kona kona nyingi, kwa mujibu wa mashuhuda wamesema dereva alikuwa kwenye mwendo kasi, alipofika maeno hayo, gari ikapinduka na kusababisha vifo vyo watu wanne, wanaume watatu na mwanamke mmoja, na majeruhi 42, na tukawachukua kuwapeleka hospitali ya Maweni ya Mkoa ambako wanaendelea kupata matibabu”, amesema Kamanda Otieno.
Kamanda Otieno amesema Jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia hali za majeruhi, na kwamba dereva wa basi hilo ni mmoja wa majeruhi waliopata majeraha makubwa, kwani alivunjika mkono wa kushoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment