0
Ushauri Kwa Wasichana Wenye Wapenzi ama Waume Wafupi

Wasichana waliowengi husema kuwa hawapendi kuwa kwenye uhusiano wa kimpenzi na wanaume wafupi kwa kile wanachosema kuwa hawajisikii amani wanapotembea nao barabarani.

Msichana mmoja kupitia mtandao wa kijamii aliuliza swali akieleza masikitiko yake kuhusu mpenzi wake kuwa mfupi. Katika swali hilo ambalo alikuwa akiomba ushauri kwa watu mbalimbali alisema, amekuwa kwenye uhusiano na mpenzi wake huyo kwa muda wa miezi sita sasa. Mpenzi wake huyo anampenda na wanaishi kwa amani, lakini tatizo ni kwamba ni mfupi.

Msichana huyo alisema mambo mengine yapo sawa, lakini huwa hana amani anapokuwa naye nje kwa sababu watu humuangalia sana, na wakati mwingine huchekwa na wapita njia. Alisema kuwa anavutiwa na mwanaume huyo, lakini ufupi ni tatizo linalomnyima amani kila saa akimfikiria.

Alikuwa akiomba ushauri ni namna gani ataweza kufanya ili ampende mwanaume huyo jinsi alivyo na ajisikie amani anapotembea barabarani.

Watu wengi walitoa maoni yao mengi yakiwa yakumsaidia msichana huyo, lakini pia kuna jambo moja muhimu sana ambalo wengi wa watoa ushauri hawakulizungumzia.

Japokuwa tunatakiwa kuvutiwa na namna mtu anavyoonekana na namna anavyotujali katika mambo mbalimbali, lakini wakati mwingine huwa tunafanya kosa kubwa la kumhukumu mtu kutokana na anavyoonekana.

Lakini pia, mhusika katika uhusiano ndiye anapaswa kufikiria nini chenye manufaa kwake bila ya kujali watu wa nje wanasema au watawaonaje. Huwezi kujilazimisha kumpenda mtu hasa kama huyo ambaye tayari nafsi yako inatilia mashaka kimo cha umbo lake.

Kama unahusiano na mwanamke au mwanaume ambaye kimo chake kinakufanya usiwe na amani hata kutembea nae, ni vyema ukawa mkweli kwa nafsi yako na ukaepusha kupotezeana muda. Kama utandelea na uhusiano huo huku ukiwa na hofu kuhusu watu watasemaje, utakuwa unauweka uhusiano wenu katika hatari ya kutokukua vizuri, na mwisho mwenza wako atajua namna unavyomchukulia kutokana na umbo lake, na hakika jambo hilo litakuwa maumivu kwake.

Kama unaweza kuachana na kuangalia kimo chake, na kuangali namna mnavyoishi, namna anavyokujali na kuhakikishia kuwa unakuwa na furaha wakati wote, basi una nafasi ya kuwa na uhusiano wenye afya. Lakini, kama utaona maoni ya jamii yana uzito zaidi kuhusu uhusiano wenu, basi achana na uhusiano huo kwani hautakuwa na tija.

Post a Comment

 
Top