0

Kulia baada ya kushiriki ngono au kufanya mapenzi ni kawaida na hushuhudiwa sana kwa wanawake, ijapokuwa imesemekana kuwa wanaume hulia pia.

Kulingana na wataalam, kuna sababu kadhaa ambazo humfanya mwanamke kulia au kujawa na huzuni baada ya kushiriki ngono, na mojawapo ya sababu hizo ni homoni ambazo mwili wa binadamu hutoa wakati huo. 

Umewahi kushiriki mapenzi na kugundua kuwa mpenzi wako amelia tu, baada ya kipindi kirefu cha kufurahisha?

Kulingana na wanasayansi, ni kawaida.

Utafiti mwingine umeonyesha kuwa kati ya asilimia saba nukta saba na asilimia thelathini na mbili nukta tisa ya wanawake wamewahi kulia baada ya kushiriki mapenzi.

Mara kwa mara, wanaume hulia pia.


Mtaalam mmoja ameieleza hali hiyo kama 'hali ambayo mwanamke hushindwa kujidhibiti na kulia bila sababu, hasa baada ya kupandwa na raha ya kujamiana, au kufika katika upeo wa raha ya kujamiana (orgasm.)


Umewahi kudhani kuwa 'ustadi' wako ndio uliosababisha kulia kwa mwanamke baada ya kushiriki ngono? Pole sana!

Hata hivyo, mtaalam mwingine amesema kuwa ukweli wa mambo na mawazo yanayokuja punde baada ya kushiriki ngono kama woga, huweza kumfanya mwanamke kulia, ijapokuwa amesisitiza kuwa kulia kwa mwanamke baada ya kushiriki mapenzi ni kawaida!

Post a Comment

 
Top