0

Msanii @Rayvanny kutoka @wcb_wasafi amesema katika utendaji kazi wake na @diamondplatnumz ndani ya label hiyo hawajawahi kufikia hatua ya kupishana kauli katika kazi.

MuimbajMakulusai huyo anayetamba na ngoma ‘#’ ameiambia Funiko Base ya Radio Five mara nyingi mambo yanayotokea ni ya kawaida ingawa kuna mengine huonyesha kutopendezwa nayo.

“Nikikosea lazima anikoromee lakini kunikoromea hajawahi kwa sababu yeye siyo mtu wa kufokafoka lakini kitu akikukataza unajua hiki kitu hajakipenda, kwa hiyo unajua wewe hapo inabidi ujiongeze,” amesema @Rayvanny.

Rayvanny na Diamond wameshafanya ngoma pamoja inayokwenda kwa jina la #Salome, pia wamekutana katika ngoma ‘#Zilipendwa’ ambayo iliwakutanisha wasanii wote walio chini ya WCB.

Post a Comment

 
Top