0
Mafufu Kumtolea Mahari Mchumba Wake Mpya Jumamosi
MWIGIZAJI wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu, baada ya kuokoka na kuachana na mambo ya kidunia huku mkewe akimwacha, hatimaye Jumamosi hii anatarajia kumtolea mahari mchumba wake mpya, Upendo Meja atakayemuoa ndani ya mwaka huu.



Akistorisha na Za Motomoto News, Mafufu alisema kuwa, shughuli hiyo ya kutoa mahari na kumvisha pete ya uchumba Upendo itafanyika nyumbani kwa wazazi wa mwanadada huyo mkoani Mbeya na wanatarajia kufunga ndoa mwezi wa nane.


“Kwa sasa ninaanza maisha upya na mke wangu mtarajiwa, Upendo ambaye nimepewa na Mungu maana alinionesha maono juu yake, vitu vyote nilivyokuwa navyo zamani nimempa aliyekuwa mke wa awali ambaye ni mama mtoto wangu.



Kiukweli kwa sasa nina furaha sana maana licha ya awali kuwa kwenye ndoa, sikuwahi kufahia maisha ya uhusiano,” alisema Mafufu.

Post a Comment

 
Top