0

Papa Francis ameutaja unyanyasaji wa wanawake kwa ajili ya ukahaba kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

Papa aliiomba msamaha jamii kwa niaba ya wanaume waumini wa kanisa Katoliki wanaokwenda kupata huduma kwa makahaba

Papa Francis alitoa kauli yake hiyo ya dhati kabisa katika kikao cha maswali na majibu na vijana kutoka mataifa mbalimbali ya dunia waliokwenda mjini Roma

Papa alisema, "Ni uhalifu dhidi ya ubinadamu. Na unatokana na fikra mbovu kwamba wanawake lazima wadhalilishwe"

Papa Francis alisema nchini Italia kuna uwezekano asilimia takriban 90 ya wateja wanaume wanaokwenda kwa makahaba ni waumini wa kanisa Katoliki waliobatizwa

Post a Comment

 
Top