0

By Allen Kilewella
Nimeangalia Picha zinazozunguka mitandaoni za hawa mabinti mawili. Kwanza ya joyce Kiria ambaye anadai mwanaume anayetaka kutoka naye hivi sasa ni lazima alipie gharama za vitu atakavyokuwa amevaa kwa asilimia sabini (70%).

Joyce inawezekana kabisa ana machungu toka kwenye ndoa yake ya kwanza ambayo imevunjika. Katikati ya maelezo yake inaonesha amepata "request' nyingi sana tangu ijulikane kwamba ameachana na mumewe.

Lakini kwenye maelezo yake inaonekana anakazia sana kurudishiwa gharama zake kuliko mahusiano na huyo mwenye kurudisha hizo gharama. Kimanti ni kwamba yeyote mwenye kuweza kurudisha gharama kwa siku husika ndiyo atatoka naye.

Nimeona pia Video ya Wema Sepetu akiwa kwenye bwana la kuogelea. Kwanza jinsi anavyochezesha makalio yake na maneno anayoyasema na kijana aliye pembeni yake kwenye bwawa lile la kuogelea inatia kinyaa.

Nawaasa Wema na Joyce wajue kwamba maisha yao yanategemea sanaa ambayo wateja wao wakubwa ni wananchi wengi ambao hawapendi matendo na maneno ya kijinga.

Post a Comment

 
Top