0

Msanii Chemical amefunguka kuhusu picha yake iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha mwenye umbo kubwa tofauti na muonekano wake wa kawaida.

Chemical ambaye anatamba na ngoma ‘Asali’ ameiambia Bongo Dot Home ya Times Fm kuwa umbo lake siku zote lipo hivyo.

“Hata nisipoji-edit mimi bado nina wowowo kabisa, mimi mtoto wa Kihaya, fresh,” amesema.

Katika hatua nyingine Chemical amezungumzia filamu yake na Wema Sepetu na kueleza anatarajia kuitoa hivi karibuni na itakuwa kazi ya mwisho ndani ya menejimenti ya Kazi Kwanza.

Post a Comment

 
Top