Akizungumza baada ya kutoka mahakamani, Mdee amesema kwamba kitendo cha kukalishwa zaidi ya masaa saba kituo cha polisi siyo jambo la kufurahisha hata kidogo huku ikizingatiwa kwamba wao ni viongozi wa wananchi hivyo ni kama usumbufu kwao kuitwa na kukalishwa.
"Tangu asubuhi tumekalishwa tu, aliyechukuliwa maelezo ni Katibu Mkuu peke yake wengine tumekaa tuu pale kwenye korido. Kutuita na kuendelea kusubiri maagizo kutoka juu ina maana hamjajipanga na huu ni usumbufu wetu," Mdee.Ameongeza "Wametuambia turudi tena Jumanne na ni matumaini yetu siku hiyo watakuwa wamejipanga na kama itakuwa mambo ni kama haya tena itafika mahali tutachoka na hatutakuja,".
Kwa upande wa Mbunge wa Tarime Mjini Esther Bulaya amesema kitendo cha viongozi wenye kutumikia wananchi kuitwa polisi kisha kupotezewa muda wa nusu siku kitendo hicho kwake anakitafsiri kama dharau.
Post a Comment