0
Wabongo Kibongo Wamuombea Msamaha Daimond kwa Zari
Wakati rais wa WCB, Diamond Platnumz akiwa busy na maandalizi ya uzinduzi wa Wasafi Redio na Wasafi TV, mashabiki wa muimbaji huyo bado wanaendelea kumbembeleza aliyekuwa mama watoto wa muimbaji huyo, Zari The Bosslady arudishe moyo nyuma.

Zari na Diamond

Mfanyabiashara huyo wa kike machachari Afrika Mashariki alimuacha baba watoto wake, Diamond kwa madai amekuwa ni mwanaume ambaye amekuwa akimzalilisha na kumkosea heshima.

Katika siku ya wapendanao, Zari aliandika ujumbe mzito wakumuachana Diamond hali ambayo aliwashtuwa watanzania wengi hasahasa mashabiki wa Diamond.

Diamond mpaka sasa hajazungumza chochote juu ya hilo lililotokea, lakini mashabiki wake wameamua kumuombea msamaha muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya muziki.

Huu hapa chini ni ujumbe wa mashabiki hao kwa Zari waliouandika kupitia mtandao wa kijajii wa Instagram.

aminamoha10

Zari mrudie tu Diamond hakuwa na nia mbaya ndio maana ilikuwa hadharani sema midomo ya watu na media inatia sana chumvi ili miachane, angalia hata ile kumbatio Diamond alikuwa kama hana ushirikiano wa kutosha, mengine ni hali ya ubinadamu lazima yatokee. Wanaume wote nadhani ni sawa ila wanashangilia tu yawenzao, Hamna hata mmoja atakaesema hana mchepiko. Unakaa South yeye anakaa Dar lakini still anajiproud kwako kuwa ndio mke akupendae, usione nyumba hizi mnalaa wote kila siku but utasikia Leo hapa kesho kule ilimradi tafarani. Huwezi sema ukimwacha utakua mwenuewe si kweli, je uendako mwenzako kwa nini alikimbia? Anakuja kwako kwa nini? Zimwi likujualo halikuli likakwisha please think twice

amuru_tanzania

Please shemeji Zarinamond do not hesitate to say NO with a big NO, learn to say no in small letters, go back to your gentleman.

mrlv3462

U look so petty but mnapendeza xna ukiwa na baba watoto wako mond

sihakaadam

Acha ujinga ww, rudi kwa mwenzio muelewane mulee watoto wenu, mm naamini wanaume unawajua vizuri tu…. Cha msingi piga moyo konde rudi muelewane basi maisha yaende… Musiwape maneno wapambe nuksi…. Ujinga wala afi mtu

tiridentebe

Mamy naomba umsamehe jmn

paulinafaustin

Zari maisha ni safari ndefu sana hebu jaribu kutuliza akili yako utafakari kwa kina hata wazazi wetu walipitia mapito kama yako lakini walivumiliana mpaka hapa walipofikia kwahiyo maisha ya ndoa yanamisukosoko piga moyo konde ili muweze kulea watoto wenu kwa pamoja hakuna binadamu mkamilifu.

Post a Comment

 
Top