0

KENYA: Kiongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Meru, Evans Njoroge ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi jana Februari 27, 2018 katika maanadamano chuoni hapo
-
Wanafunzi hao waliandamana wakishinikiza Chuo hicho kupunguza ada kwa kiasi cha shilingi 8,500 za Kenya ambazo ni sawa na Tsh 188,566 na kuboreshewa miundombinu chuoni hapo
-
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho baada ya vurugu walikimbia nje ya chuo na kwenda kujificha mashambani baada ya kuona gari la Polisi
-
Shuhuda mmoja alisema kuwa maaskari baada ya kuwakosa chuoni walienda uraiani kuwatafuta, alisema mtoto mmoja aliwaelekeza Polisi wanafunzi hao walipojificha
-
Shuhuda huyo alisema alisikia mlio wa bunduki na alipotoka alimkuta askari anabadilisha mavazi yake na kubakia na nguo za kiraia
-
Kwa upande wa mashuhuda wengine wamesema kuwa polisi huyo aliyemuua mwanafunzi anafahamika ni Afisa wa jeshi la polisi la kituo cha Nchiru.

Post a Comment

 
Top