DAR: Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(FGBF), Zachary Kakobe akana Kanisa lake kukwepa kodi adai tuhuma hizo ni za kisiasa
Siku 5 zilizopita Kamishna Mkuu wa TRA aliwaambia Wanahabari kuwa baada ya uchunguzi wamebaini kuwa Askofu Zachary Kakobe hana akaunti wala fedha katika Taasisi yoyote ya fedha hapa nchini
Aidha uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa(Signatories) zenye jumla ya kiasi cha shilingi biloni 8.
Uchunguzi wa TRA ukaonesa kuwa Kanisa hilo Iilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza mitaji. Kodi hiyo ililipwa baada ya uchunguzi.
Mnamo mwezi Disemba mwaka 2017 Askofu Kakobe aliingia katika mgogoro na Serikali kwa sababu zinazodaiwa kuchochewa na kauli zake zenye utata kwa Rais Magufuli pamoja na kukosoa mwenendo wa hali ya siasa nchini
Post a Comment