0
Lowassa, Njoolay Watupilia Mbali Tuhuma za Kigwabgalla ..... Sumaye Ahaidi Kumfikisha Mahakamani
Familia ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Sumaye na  na Njoolay imetupilia mbali madai yaliyoelekezwa kwake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kingwangalla, jana.

Katika madai yake aliyoyatoa wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Njiro mjini hapa, Dk. Kigwangalla alidai Lowassa ni sehemu ya watu waliojipatia eneo katika eneo la mamlaka hiyo.

Msemaji wa familia ya Lowassa, Fredrick Lowassa, alitupilia mbali madai yaliyotolewa na Dk. Kigwangalla huku akisema familia yao inatambua kumiliki eneo hilo kihalali.

Akizungumzia tuhuma hizo Sumaye huku akicheka alisema, “...Nitampeleka mahakamani. Nyinyi cha kufanya andikeni hicho alichokisema vizuri ili nimpeleke mahakamani. Sina nyumba yoyote Arusha sasa kama anadhani yeye kazi yake ni kuwachafua watu acha aendelee, nampeleka mahakamani.”

Fredrick katika ujumbe wake alioutoa mara baada ya baba yake(Lowassa) kutajwa alisema, “Nimesikia taarifa za Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha.”

Alisema amesikitishwa na matamshi hayo akisema hakutarajia kutolewa na mtu mwenye wadhifa wake.

Alisema Dk Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais John Magufuli kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina wataalamu wenye uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote.

“Nikiwa kama msemaji wa familia ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa,” alisema,

“Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Kigwangalla hayapo na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu.”

Baadaye waziri huyo alimjibu mtoto huyo wa Lowassa akisema, “Mdogo wangu Fredrick Lowassa, tulia usiwe na hofu. Sikukurupuka kuhusu issue ya mzee wako, Ndg. Edward Lowassa, kama ana kiwanja ama la, kwenye eneo la Plot No. 4091 Njiro Arusha.

"Ukweli ni kwamba nilichokisema ni kuwa ‘tusubiri tupate majibu toka kwa mamlaka inayohusika na kutoa hati za umiliki wa ardhi kwa sababu kuna majina mengi makubwa yanasemwa... Hatuwezi kuwahukumu ama kuwataja waziwazi kwa sasa mpaka tupate nyaraka maana inawezekana wanasingiziwa.”

Njoolay, ambaye pia amewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Mwanza na Rukwa alisema, “Nimesikitishwa sana na tamko la waziri. Niliwahi kuwa kiongozi serikalini, siwezi kuwa mvamizi kwa sababu Jiji lilitangaza viwanja na sisi tukaomba na kupatiwa kama wananchi wengine.

"Kigwangalla kama alitaka kupata ukweli angekutana na sisi kwanza. Akitaka kupata ukweli aunde kamati ndogo ambayo itabaini ukweli. Kusikiliza kabla ya kutuhumu ndio utawala bora. Tunajua Serikali haifanyi kazi kwa matamko kama suala hili lipo tunasubiri barua kutoka serikalini.”

Post a Comment

 
Top