0
Kiukweli awamu ya nne ya Jakaya Kikwete wapinzani mlidekezwa sana ikajengeka baadhi miongoni mwenu tabia ambazo si njema kwa maadili ya kitanzania. Dharau kwa mamlaka, kejeli, matusi, dhihaka na mengineo mengi yenye kuikera jamii ya wastaarbu.

Hili lilichagizwa na kupewa nguvu na baadhi ya vijana waliotumika katika maandamano ya kila mara yasio na tija kwa taifa.

Kipindi cha awamu ya nne ya Jakaya Kikwete baadhi ya wanasiasa wa upinzani walitumia uhuru huo vibaya. Waliposhikiliwa na vyombo vya dola, walitumia makundi ya vijana kuvamia vituo vya polisi kulazimisha waachiwe. Hii kwa waliokua hawajitambui iliwapa kiburi Sana.

Zama zimebadilika kabisa Serikali hii imejikita kurudisha nidhamu iliopote kwa wanasiasa na watumishi wa umma ikijikita kutumikia wananchi ambao upinzani kwa muda mrefu ulituhumu wamepuuzwa.

Kwa sasa vijana na makundi mbalimbali wameelewa dhamira ya dhati ya awamu ya tano katika kuwaondelea kero zilizopigiwa kelele kwa muda mrefu na upinzani.

Kujua hili, hapo nyuma angekamatwa Sugu vijana wa Mbeya wangeandamana aachiwe kwa vurugu nyingi lakini wamemchoka na kumpuuza. Kwa sasa yuko ngomeni na hali ya mji wa Mbeya ni tulivu.

Hali kadhalika kwa Lema, ile miezi minne hatukuona maandamano ya kutaka aachiwe, wamemchoka na kumpuuza. Vijana wako busy wanapambana na shughuli za kujitafutia kipato, wamechoka kutumika pasi na Faida yoyote.

Hili ni funzo kwa wanasiasa model ya watajwa hapo juu.

Wataishia kuilaumu Serikali wakati wao binafsi wanashindwa kutimiza wajibu wao, wanaishi kwa mazoea.

Kikwete aliposema mtamkumbuka mlipomwita dhaifu alimaanisha jambo, sasa mnaona jinsi alivyowadekeza.

Badilikeni, muda bado mnao wa kutosha kwenye uhai wenu, kwani mngali vijana

By thetallest

Post a Comment

 
Top