Badala ya sherehe za Uhuru, tumefanya usafi ili kupambana na kipindupindu, na fedha zilizookolewa zinajenga sehemu ya barabara iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi.
Badala ya Rais na Wabunge kujipongeza kwa sherehe kubwa, fedha zilizookolewa zimetatua tatizo la vitanda kwa wagonjwa.
Badala ya sherehe za siku ya UKIMWI, fedha zimekwenda kununua dawa za kufubaisha makali ya UKIMWI.
Badala ya semina elekezi ya Mawaziri, fedha zake zitakwenda kutekeleza mradi wa kufunga vifaa vya kisasa vya kuchunguza magonjwa katika hospitali 37 kote nchini.
Badala ya safari za nje fedha zilizookolewa zitatumika kwenye miradi ya maendeleo. Zaidi ya Sh.7 bilioni ambazo zingeweza kutumika kwa safari za nje zimeokolewa katika siku 100 na zitatumika kwenye miradi hiyo ya maendeleo.
Hatua hizo, na nyingine nyingi, zimevuta hisia za watu mbalimbali kote duniani. Mnaofuatilia mitandao ya kijamii mnajua hivyo, na wapo wameonesha wazi kutamani tungewaazima Rais wetu kwa muda" Alisema Balozi Ombeni Wakati akitoa Tasmini ya Siku 100 za Rais Ikulu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment