0
Baada ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kuufungia wimbo mpya wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’ na kudai kushangazwa na baadhi ya radio kuanza kuupiga wimbo huo na baadae kuwataka BASATA wafafanue kuhusu uhalali wake, Idara ya muziki wa EATV na East Africa Radio imetolewa ufafanuzi swala hilo.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Mkuu wa idara ya muziki kutoka EATV na East Africa Radio, DJ Bigman ‘Kim’ amedai wimbo wa Nay ‘Shika Adabu Yako’ hauna matusi.

“Sisi kama East Africa Radio na EATV tuna utaratibu wetu, kuna kitengo kabisa cha muziki ambacho kinaitwa ‘Music Committee’. Kamati ya muziki kazi yoyote mpya inayokuja kwenye radio na TV kazi yetu ni kuiangalia na kuhariri. Tukiona kama nyimbo ina ukakasi, tunawasiliana na msanii either atuletee nyingine nzuri ambayo itakuwa kwa ajili radio au atupe ruhusa ya sisi kuhariri kwa vile ambavyo tutaona inafaa. Kwa sababu tunajua kwamba msanii anakuwa na fans wake na wale fans wanahitaji kitu kutoka kwake, kwahiyo tunaona ile nyimbo kutokwenda hewani tunamnyima haki msanii. So kwa issue kama hii sisi tumeusikiliza wimbo, tumeona ni wimbo mmoja kama ni controversial fulani lakini hajatukanwa mtu, hakuna neno lolote la kumtusi mtu, yaani ni kama comedy fulani hivi, kama rap katuni hivi imetungwa ambayo imewekwa katika mtiririko mzuri. Kwa mimi binafsi ninaweza sema hii kama imeishtua game, game kama ilikuwa imelala. Yaani zinahitaji vitu kama hivi ili watu wapate kufunguka,” alisema DJ Kim.

Post a Comment

 
Top