0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema amekaa kimya kwa muda mrefu kuhusiana na suala la Zanzibar kwa sababu Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar ni huru na hawezi kuiingia kwa namna yoyote.

Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Diamond Jublee jijini Dar es salaa alipokuwa akilihutubia taifa kupitia mkutano ulioandaliwa na wazee wa Jiji la Dar es salaam.

''Zanzibar ina tume yao ya uchaguzi (ZEC) kama ilivyokuwa Tanzania bara tulivyo na (NEC) hivyo kama kuna ambaye hajaridhika na hali hiyo aende mahakamani mahakama ndiyo itakayotoa tafasiri'' amesema Dkt. Magufuli.

Rais ameongeza kuwa ataendelea kukaa kimya kuhusu Zanzibar ili wajiendeshe wenyewe kumaliza uchaguzi wao kama Tanzania bara tulivyomaliza uchaguzi wetu salama.

Aidha Rais amesema yeye kama Amiri Jeshi mkuu hatakubali chokochoko yoyote Zanzibar au katika eneo lolote la nchi na yeyote atakaye jaribu kuleta vurugu vyombo vya usalama vipo makini na vitahakikisha amani na usalama wa nchi unadumu siku hadi siku.

Post a Comment

 
Top