0
Mtayarishaji wa muziki anayetamba kwa sasa,Nahreel kutokea studio ya The Industry amesema kuwa mwaka 2015 ndio umekuwa wa neema kwake kwani ndio mwaka ambao pochi lake limetuna sana kwa kutengeneza mkwanja mrefu zaidi kwenye tasnia hiyo kuliko miaka mingine yote huku akitingisha mawimbi ya redio kwa hits zaidi ya 16 kutokea mikononi mwake.

Nahreel amesema kuwa mwaka jana ameweza kupata nafasi ya kushiriki kwenye coke studio nchini kenya ambapo alikatiwa mkwanja unaovutia pia ukitoa kazi za studio ameweza kupata deals za matangazo nyingi.

“kweli,muziki unalipa na mimi kama producer umenilipa kwa njia nyingi,kwa wasanii kunilipa studio,kwa kazi nazopata off studio.Mwaka 2015 nilihusika kwenye coke studio nililipwa hela nzuri,nilipata radio adverts za makampuni tofauti..as producer nimenufaika sana mwaka 2015 kuliko miaka mingine yote" alifunguka producer huyo ambaye pia ni msanii wa navy Kenzo.

Post a Comment

 
Top