0

Chama cha APPT Maendeleo, kimetangaza rasimi kwamba hakitashiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio kutokana na kupoteza imani na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), baada ya kufuta kibabe matokeo ya

uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana.

Msimamo wa APPT ulitolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Peter Kuga Mziray katika barua yake kwa  (ZEC), ambayo nakala yake ilisambazwa kwa vyombo vya habari Zanzibar.

APPT kinakuwa chama cha pili kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo wa Machi 20 baada ya Chama kikuu cha upinzani Zanzibar, CUF kutoa tamko lake kama hilo mwezi uliopita.

Mziray alisema njia iliyotumiwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi haikuwa ya kisheria hivyo APPT Maendeleo haitambui kufutwa kwa uchaguzi huo.

Post a Comment

 
Top