0
Mmoja wa wapinzani wakuu katika uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamis wiki hii nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye, amepinga matokeo ya uchaguzi huo.

Dkt. Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Ijumaa amesema kuwa raia nchini Uganda wameshuhudia udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huo, ambao haujahi kufanyika katika taifa hilo.

Kanali huyo mstaafu ameuelezea uchaguzi huo kuwa si halali na kuwa ni sawa na mapinduzi ya kijeshi.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana, Rais wa muda mrefu wa taifa hilo Yoweri Kaguta Museveni, alitangazwa mshindi.

Rais Museveni ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka thelathini sasa, alipata zaidi ya asilimia 61 ya kura huku Besigye akijipatia asilimia 35 ya kura.

Waangalizi wa kimataifa wamesema kuwa uchaguzi huo uliandaliwa katika mazingara ya hofu na kudhalalishwa.

Post a Comment

 
Top