0
Zikiwa zimepita siku chache tangu waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam na kubaini uozo wa kuchepushwa kwa bomba la mafuta mamlaka hiyo imekuja na mpango madhubuti wa kuimarisha usalama katika bandari hiyo kwa kufunga mfumo mpya wa kamera 486 zenye uwezo wa kuonyesha matukio yote yanayotokea nje na ndni ya bandari hiyo na hasa katika eneo la kupakulia mafuta.

ITV ilifika bandarini hapo na kushuhudia namna kamera hizo zinavyofanya kazi huku afisa mlinzi mwandamizi Bw Kiswiza Lukasi akielezea namna mashine hizo zinavyofanya kazi.

Naye Bi Janeth Ruzangi meneja mawasilino wa TPA amesema mashine hizo zinaonganisha na banadari zote lengo ni kuakikisha kuwa usalama unaimarika katika bandari za hapa nchini.

Baadhi ya watumiaji wa bandari hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia utendaji na usalama wa bandari hiyo lakini kwa sasa wanapata imani kuwa mali zao zitakuwa salama.

Post a Comment

 
Top