Kufichuka kwa kashfa za ufisadi katika Bandari kumedhihirisha namna serikali inavyopoteza mabilioni ya shilingi kupita Bandari ya Dar es Salaam pekee kutokana na uzembe na ufisadi wa watendaji.
Mapato yanayopatikana katika Bandari ya Dar es Salaam ni mengi mno kiasi kwamba kama serikali inakusanya na kusimamia kwa makini, hata maendeleo yanaweza kuonekana na hakutakuwa na haja ya kutegemea misaada ya wahisani ambayo mara nyingi ni ya kujidhalilisha.
Lakini bandari ya Dar es Salaam ni miongoni mwa bandari karibu 10 muhimu zilizopo nchini Tanzania, ambazo ‘zimetelekezwa’ na serikali na hivyo kuikosesha mapato mengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment